WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa Halmashauri na Mji wa Bunda
pamoja na Madiwani washirikiane katika utekelezaji wa ujenzi wa miradi
ya maendeleo.
Pia
amewaagiza watumishi wa umma katika halmashauri ya wilaya na mji wa
Bunda wafanye kazi kwa bidii na wawahudumie wananchi bila ya ubaguzi wa
aina yoyote.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo jana (Ijumaa, Januari 19, 2018) wakati akizungumza
na watumishi na Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya na wa Halmashauri Mji
wa Bunda, katika ukumbi wa Halmashauri ya Bunda.
“Watumishi
wa umma acheni kukaa sana maofisini tengeni muda wa kuwatembelea
wananchi katika maeneo yao na shirikianneni nao katika kutatua kero
zinazowakabili. Madiwani na watumishi lazima mshirikiane ili kuwaletea
wananchi maendeleo.
Alisema
watumishi na madiwani wakishirikiana katika usimamizi wa utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo, wilaya itafanikiwa katika maendeleo ya
kijamii na kiuchumi.
Pia
Waziri Mkuu aliwasisitiza watumishi hao kufanya kazi kwa mujibu wa
sheria na taratibu za utumishi na wajiepushe na vitendo vya rushwa,
wizi , ufisadi na uzembe kwa sababu vinarudisha nyuma maendeleo ya
wananchi.
Awali,
Waziri Mkuu alikagua mradi wa maji wa Bunda na baadae alizindua kikundi
cha Ushirika cha Igembe Sabo na kukagua skimu ya umwagiliaji wa zao la
mpunga ya Nyatwali wilayani Bunda.
Waziri
Mkuu alihitimisha ziara yake wilayani Bunda kwa kuhutubia mkutano wa
hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Stendi Mpya katika mji mdogo wa
Bunda.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
0 comments:
Post a Comment