WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amewaasa wanaume wa wilaya ya Tarime kujiepusha na
vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na kuachana na
kilimo cha bangi.
Alitoa
kauli hiyo jana jioni (Jumatano, Januari 17, 2018) wakati akihutubia
wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa
Serengeti, wilayani Tarime.
Waziri
Mkuu alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto pamoja na
kilimo cha bangi vinaitia doa wilaya hiyo, hivyo hawana budi wakaepukana
navyo.
“Serikali
inakemea vitendo vya ukatili, achaneni navyo. Mtu unamchapa mtoto
makofi hadi anazimia, kitendo hicho hakiwezi kuvumilika na pia kinaitia
doa wilaya yenu.”
Wakati
Huo huo, Waziri Mkuu alimuagiza Mkuu wa wilaya hiyo, Bw. Glorious Luoga
kuendelea na msako wa mashamba ya bangi na mirungi na kuchukua hatua
kwa watakaobainika kuendesha kilimo hicho.
Alisema
ardhi ya wilaya hiyo ni nzuri na inahimili kilimo cha mazao mbalimbali
ya chakula na biashara kama mahindi, mihogo, ndizi, kahawa, pamba, ni
marufuku kulima bangi.
Pia
Waziri Mkuu aliagiza kuchukuliwa hatua kwa wakandarasi waliotekeleza
ujenzi wa maji mkoani Mara kwa sababu miradi hiyo wameijenga chini ya
kiwango.
Waziri
Mkuu aliyasema hayo baada ya kupokea malalamiko ya wananchi kupitia
mabango wakidai kutonufaika na miradi ya maji katika maeneo yao licha ya
Serikali kutoa fedha.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
0 comments:
Post a Comment