Home » » Jeshi la Polisii Lakanusha Habari ya NIPASHE Kuhusu Kuwakama Wavaa Vimini, Milegezo na Wanyoa Viduku

Jeshi la Polisii Lakanusha Habari ya NIPASHE Kuhusu Kuwakama Wavaa Vimini, Milegezo na Wanyoa Viduku

Unknown | Thursday, January 18, 2018 | 0 comments

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limekunusha taarifa ya kukamata watu wanaovaa vimini na kunyoa mtindo wa kiduku.

Hatua hiyo inakuja baada ya gazeti la kila siku la Nipashe January 17 (jana) kutoka na kichwa cha habari; Polisi yakamata wavaa vimini, kunyoa viduku.

 
Akizungumza jana Dar es Salaam, Kamanda wa kanda hiyo, Lazaro Mambosasa alisema taarifa hiyo haina ukweli wowote kwani mwandishi ameandika kitu ambacho hakukisema.

“Nilitaka nitoe ufafanuzi nikikanusha haya ambayo yameandikwa hayakusemwa na Jeshi la Polisi, ameyasema mwenyewe mwandishi kwa interest yake na sana alichokuwa anatafuta ni umaarufu wa stori.


Mambosasa alisema hakuna sheria yoyote inayowazuia watu kuvaa nguo fupi na kwamba alichokisema Rais Magufuli ni kwamba anachukizwa na wasanii wanaovaa nusu uchi na kuoneshwa katika vituo vya Runinga,kitu ambacho ni kinyume na maadili yetu.

"Kwa kuwa jambo hilo  ni machukizo na halivunji sheria za nchi ni vigumu  kwa Polisi kuanzisha msako, labda watu hao tuwakute wakifanya biashara ya ukahaba." Alisema Mambosasa na kuongeza;

“Ninamtaka sasa mwandishi arudi kwa watanzania aombe radhi ili kuondosha usumbufu uliojitokeza, nimepigiwa simu kuanzia jana(juzi) toka maeneo mbali mbali kwa jambo ambalo kimsingi halijafanywa na Jeshi la Polisi.”



==>Msikilize hapo chiniakiongea

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG