Home » » Waziri Mahiga akutana na Kamati ya kuchunguza mauaji ya wakulinda amani DR Congo

Waziri Mahiga akutana na Kamati ya kuchunguza mauaji ya wakulinda amani DR Congo

Unknown | Sunday, January 14, 2018 | 0 comments
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Dkt. Augustine Mahiga amekutana na kufanya mazungumzo na wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa ya kuchunguza mauaji ya askari wa kulinda amani nchini DR Congo.

Wanajeshi hao walipoteza maisha  wakiwa nchini DRC katika jukumu lao la kulinda amani ambapo Askari hao waliouawa wakiwa katika operesheni ya ulinzi wa amani chini ya Umoja wa Mataifa nchini Congo- DRC.

Miili ya wanajeshi hao iliwasili nchini Jumatatu Disemba 11 na kisha kupelekwa katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo. Miili hiyo iliagwa Disemba 14 katika viwanja vya Makao Makuu ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga jijini Dar es Salaam. Mbali na hao waliouawa, wengine zaidi ya 40 walijeruhiwa

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG