WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa ameitaka Wizara ya Nishati ijiridhishe na ubora wa
vifaa vinavyotumiwa na wakandarasi katika miradi ya umeme.
Pia
iwasimamie wakandarasi hao kwa ukaribu ili kuhakikisha thamani ya
miradi inayotekelezwa inalingana na kiasi cha fedha wanacholipwa
wakandarasi hao.
Ametoa
kauli hiyo jana (Jumamosi, Januari 13, 2018) wakati akizungumza katika
kikao cha maendeleo ya usambazaji umeme kilichofanyika , Ofisini kwake,
Dodoma.
Waziri
Mkuu alisema wakati huu ambao Wakala wa Nishati Vijijini (REA)
wakiendelea na miradi ya usambazaji umeme, ni vema wizara hiyo
ikajiridhisha na ubora wa vifaa.
“Wasimamieni
wakandarasi kikamilifu na kama hamjaridhishwa na kazi wanayofanya
msisite kuwachukulia hatua, tunataka wananchi wapate umeme.”
Alisema
Rais Dkt. John Magufuli amedhamilia kuona umeme unasambazwa kwenye
vijiji vyote nchini kwa lengo la kuboresha maendeleo ya wananchi.
Hivyo,
Waziri Mkuu amesisiza kwamba ni lazima wakandarasi waliopewa jukumu
hilo wasimamiwe kikamilifu ili mradi hiyo iweze kuwa na ubora
unaostahili.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani amesema tayari
wakandarasi wanaotekeleza mradi wa REA namba tatu wameshaanza kazi.
Amesema kwa wakandarasi ambao bado hawajaanza wamekubaliana kwamba wataanza wakati wowote na wa mwisho ataanza Machi 2, 2018.
Dkt.
Kalemani amesema wizara yake itahakikisha miradi yote ya kusambaza
umeme inasimamiwa kikamilifu na inakamilika kwa wakati na katika ubora
unaostahili.
Kikao
hicho kilihudhuliwa na Waziri wa Nishati Dkt.Kalemani, Naibu Waziri wa
Fedha na Mipango Dkt. Ashatu Kijaji, Naibu Waziri wa Nishati Bibi Subira
Mgalu, Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Bibi Maimuna Tarishi.
Wengine
ni pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Naibu Katibu Mkuu wa
wizara hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya REA, Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO,
Mtendaji Mkuu wa REA, Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO, Kamishna
Msaidizi-Bajeti.
0 comments:
Post a Comment