Home » » Watu 40 Watiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Mauaji ya Watu Wawilii

Watu 40 Watiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Mauaji ya Watu Wawilii

Unknown | Sunday, January 14, 2018 | 0 comments
Jeshi la Polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu zaidi ya  40, wakazi wa Kijiji cha Mikomariro wilayani Bunda kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili sababu ikitajwa kuwa ni mgogoro wa mpaka wa shamba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed amethibitisha kukamatwa kwa watu hao huku akiongeza kuwa Jeshi lake bado linawasaka watu wengine waliohusika na tukio la mauaji ya watu wawili wakazi wa Kijiji cha Remng'orori wilayani Serengeti.

Aidha kamanda Jafari amebainisha kuwa waliokamatwa ni wale walioshiriki yowe iliyosababisha mauaji ya watu wawili kwa kuwakata kwa mapanga kwa sababu ya ugomvi wa mipaka ya mashamba.

Amesema kuwa chanzo cha mgogoro huo ni mpaka wa wilaya za Bunda, Serengeti na Butiama ambao unahusisha eneo la ekari 3,535 ambapo Wegesa Gikene na Nyamhanga Gembo wakazi wa Kijiji cha Remng'orori waliuawa kwa kukatwa na mapanga wakati wakiwa shambani.

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG