Shirika
la Fedha la Kimataifa (IMF) ijumaa hii limeonya kuhusu kupungua kwa
kasi ya ukuaji wa uchumi wa Tanzania, likisema kuwa serikali inafaa
kuchukua hatua za haraka ili kubadilisha mwelekeo wa kushuka.
Katika
taarifa yake mpya kuhusu uchumi wa Tanzania, IMF imesema kuwa, licha ya
kuwa takwimu za pato la taifa kuoyesha kukua, lakini takwimu ningine za
uchumi zinaeleza kudorora kwa shughuli za kiuchumi. Taarifa hiyo
imetolewa baada ya kukamilisha mapitio yake ya Sera za Kukuza Uchumi PSI
kuhusu Tanzania.
Ukusanyaji
wa mapato umekuwa mdogo kuliko ulivyotarajiwa na ongezeko la alama za
imani limekwama katika baadhi ya mabenki kutokana na kuongezeka kwa
mikopo mibaya.
Kumekuwa
na athari mbaya kwenye ukuaji wa uchumi katika kipindi kifupi kutokana
na utekelezaji mdogo wa bajeti, ulioleta changamoto kwenye mazingira ya
kibiashara, na sekta binafsi ikilalamika kubanwa sana na sheria.
Uchumi
wa Tanzania katika kipindi cha muongo mmoja uliopita ulikuwa unakua kwa
asilimia 7 kwa mwaka, lakini mwezi Novemba Benki ya dunia ilitangaza
kuwa kasi hiyo huenda ikapungua hadi asilimia 6.6 mwaka jana
0 comments:
Post a Comment