Jumla
ya wanafunzi watano wa kike wa shule za sekondari Tandahimba waliopata
mimba mwaka 2017 wamekamatwa pamoja na wazazi watano baada ya kufanyika
msako na kufanikiwa kukamatwa kwa watu hao.
Katibu
Tawala wa wilaya ya Tandahimba, Mohamed Azizi amesema hayo jana
Jumamosi kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, Sebastian Waryuba baada ya
kufanikiwa kuwakamata wanafunzi hao wakiwa na watoto wao huku wahusika
ambao wamewasababishia kukatiza masomo yao kutokomea kusikojulikana.
“Tumefanikiwa
kuwakamata wazazi na wanafunzi watano wakiwa wamejifungua kati yao
mmoja ameacha shule akiwa kidato cha nne, huku mwingine tatu na kidato
cha pili baada ya kuzungumza nao wote wamesema hakuna hata mmoja ambaye
anapata huduma kutoka kwa wahusika ambao wamewapa mimba hali ambayo
inawapa shida wazazi wao kuwahudumia,” alisema Azizi
Kwa
upande wake Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkolea, Selemani Abduli amesema
baada ya kupata taarifa kutoka kwa mkuu wa shule hatua ambazo
amezichukua ni kuwakamata wahusika wote wawili na kuwapeleka katika
kituo cha polisi kilichopo wilayani humo.
“Hatua
ambayo nilichukua baada ya kupata taarifa kwa wakuu wa shule ni
kuwatafuta wanafunzi ambao wamepata ujauzito pamoja na wahusika
kuwapeleka kituo cha polisi lakini wahusika wakifika kituo cha polisi
waliachiwa,” alisema Abdul
Akizungumzia
tukio hilo mmoja wa mzazi ambaye mwanaye amekatiza masomo yake kutokana
na kupata ujuzito Hassan Mfaume amesema amesikitishwa baada ya kusikia
mwanaye amepata ujauzito hali ambayo imepelekea kukatiza masomo yake.
0 comments:
Post a Comment