WAZIRI
wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George
Mkuchika amesema kuwa, ofisi yake haiungi mkono mfumo wa kazi kwa
mikataba.
Waziri
Mkuchika ameongeza kuwa, mfumo huo ni gharama kubwa ukilinganisha na
kuajiri mfanyakazi kwa ajira ya kudumu na kwamba wizara yake
inashughulikia suala hilo na kwamba hivi karibuni taasisi za umma
hazitaruhusiwa kuajiri wafanyakazi wapya kwa mfumo wa mikataba.
“Tunataka
kila ofisi kuajiri kwa mujibu wa mahitaji, hatutaruhusu mfumo huu wa
mikataba kuendelea kwa sababu ni gharama kubwa mno kwa serikali,”
alisema.
Kuhusu
wafanyakazi wanaokwenda likizo maalum, waziri alisema yeyote
atakayekwenda katika likizo ya namna hiyo atatakiwa kuwasilisha nyaraka
zake wizarani lini anarudi na wale watakaowasilisha barua kuwa wamerudi
wanatakiwa kusubiri jibu la serikali.
“Kama
ulikuwa nje ya nchi au ofisi mfano miaka mitano, ni dhahiri kuna mtu
alijaza nafasi yako, hivyo unaporudi, unatakiwa kuwasilisha barua na
kuipa nafasi serikali kujibu,” alifafanua Waziri Mkuchika.
Ameeleza
kwamba, suala la likizo maalum sio jambo jipya katika mfumo wa
utumishi wa umma na umekuwa ukitumika katika nchi nyingi duniani
“Hatuna shida nayo, lakini tunataka wafuate taratibu sahihi wanaporudi.”
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuchika amesema kuwa, Bodi ya Mishahara na
Maslahi (HSRB) iko katika hatua za mwisho za kurekebisha mfumo mzima wa
mishahara, utakaondoa tofauti ya uwiano wa mishahara katika taasisi za
umma kwa wafanyakazi wenye ujuzi, sifa na uzoefu.
0 comments:
Post a Comment