Serikali
imelazimika kusogeza mbele tarehe ya kufungua shule kwa shule za
Azania, Jangwani na Milambo kutokana na Wakala wa Majengo(TBA),
kushindwa kumaliza ukarabati huo kwa muda uliotakiwa.
Uamuzi
huo ulifikiwa jana Jumamosi jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Leonard Akwilapo alipokutana na
walimu wa shule hizo na viongozi wa Manispaa ya Ilala.
Akwilapo
alisema kitendo hicho hakijamfurahisha na kuahidi kufuatilia kwa mara
nyingine mkataba wa namna ya utekelezaji wa ukarabati huo walioingia
Wizara na TBA.
"TBA
mnapaswa kujua mmepewa jukumu hili kwa kuwa Serikali imewaamini, lakini
hii isiwe kisingizio cha nyie kuvurunda kwa kisingizio tu ni taasisi ya
Serikali nitapitia tena upya na mwanasheria wetu mkataba tulioingia
kuona ni wapi watu hawakutekeleza wajibu wao na hatutasita kuchukua
hatua tutakapobaini kuna tatizo," alisema.
Hata
hivyo, alisema pamoja na kuongeza siku hizo ambapo sasa badala ya
kufungua shule kesho Jumatatu, watafungua Januari 22, hataongeza siku
zaidi na kuwahakikishia walimu kwamba muda walioupoteza wa ratiba za
kufundisha zitafidiwa katika likizo ya Aprili na ile ya Juni.
Akijibu
sababu zilizowachelewesha kumaliza ukarabati huo kwa muda, Kaimu Meneja
wa TBA Mkoa wa Dar es Salaam, Manasseh Shekalaghe alisema zipo sababu
nyingi zilizochelewesha ikiwemo gharama kuongezeka tofauti na
ilivyodhaniwa awali.
0 comments:
Post a Comment