Serikali ya Uingereza imetangaza leo Alhamisi,
Januari 18 kwamba inaongeza euro Milioni 50,5, mchango wake wa kifedha
kwa eneo la Calais na pwani za Ufaransa ili kuimarisha usalama mpakani.
Tamko rasmi kabla ya ziara ya
rais wa Ufaransa Emmanuel Macron nchini Uingereza kwa mkutano wa nchi
mbili kuhusu masuala ya usalama wa mipaka na ulinzi.
Ishara ya kifedha iliyotolewa na serikali ya Theresa May inakutana na
matarajio yaliyoelezwa na Ufaransa ambayo inashtumu kwa miaka kadhaa
suala la mikataba ya Touquet, huku shinikizo la uhamiaji limeongezeka
katika Calais, ambapo uliopo mpaka wa Uingereza tangu 2004.
Euro milioni 50 iliyoahidiwa inapaswa kutumika kuboresha hatua za
usalama katika bandari ya Calais na maeneo jirani. Uingereza imetumia
euro milioni 113 katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita na kutambua
kuwa mikataba ya Touquet ni manufaa sana kwa nchi hiyo.
Hata hivyo, viongozi wengine wa Uingereza tayari wamekosoa mchango
huo kama vile Mbunge wa chama cha kihafidhina kutoka Dover ambaye
amebaini kwamba London tayari imetoa "mamilioni kwa Ufaransa" na inpaswa
kuwekeza katika usalama wa mpaka kwenye pwani za Uingereza.
Hali hii itampelekea Theresa May na Emmanuel Macron kusaini mkataba mpya ambao utakamilisha mikataba ya Touquet.
Kwa ombi la Ufaransa, London pia imekubali kuhudumia wahamiaji wengi
wanaokuja Calais, ikiwa ni pamoja na watoto wadogo. Viongozi hawa wawili
pia watajadili kuhusu masuala ya kijeshi ili kuonyesha kwamba licha ya
Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya, msikamano wa pamoja utaendelea
na utaimarishwa. Uingereza pia imetangaza kutumwa kwa helikopta tatu za
Royal Air Force na wafanyakazi ili kusaidia vikosi vya Ufaransa katika
eneo la Sahel.
0 comments:
Post a Comment