Mbunge
wa Singida Mashariki Tundu Lissu amefunguka na kusema kuwa kesho
Januari 6, 2018 atasafiri na kutoka nje ya Kenya kwenda kufanyiwa
matibabu zaidi kufuatia shambulio la kupigwa risasi lililotokea mwaka
jana.
Lissu
amesema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari akiwa nje ya
hospitali ya Nairobi na kusema kuwa amekuwepo hapo kwa takribani miezi
minne akifanyiwa matibabu lakini sasa anakwenda kufanyiwa matibabu zaidi
sehemu nyingine.
Mbali
na hilo Tundu Lissu ameendelea kusema kuwa shambulio lake kupigwa
risasi ni tukio la kisiasa ndiyo maana viongozi wa bunge wamekuwa
wakishikwa na kigugumizi.
Amesema
Bunge limeshindwa kumhudumia na kumlipia matibabu kama ambavyo inapaswa
kuwa lakini pia hakuna kiongozi yoyote wa Bunge ambaye amethubutu hata
kwenda kumuona.
"Leo
nazungumza Bunge la Tanzania halijatoa hata shilingi moja wakati sheria
ipo wazi, ndugu zangu wamewaandikia barua ya kuwaomba kupata haki ya
matibabu lakini mpaka tunazungumza sasa hivi Spika wa Bunge, Naibu Spika
wa Bunge, Katibu wa Bunge wala hakuna kiongozi wowote wa Bunge
aliyefika kuniona kwa miezi hii minne, walijua sitaweza kupona ndiyo
maana hawakuwa na Plan ya kunitibu" amesema Lissu
Aidha
Mbunge huyo ametoa maoni yake kuwa anaamini jaribio la yeye kutaka
kuuawa mnamo Septemba 7, 2017 ni jaribio la kisiasa na amedai anaamini
jeshi la polisi nchini Tanzania hawapelelezi juu ya tukio hilo.
"Maoni
yangu kilichofanyika kilikuwa ni jaribu ya mauaji ya kisiasa moja kwa
moja, mimi siyo mfanyabiashara, jeshi la polisi kwa maoni yangu
hawapelelezi tukio hili kwa sababu sijawahi ona mtu anakuja kuniuliza,
wanamtaka dereva wangu kwaajili ya kumkamata na sio kumhoji juu ya tukio
hilo" amesema Tundu Lissu
0 comments:
Post a Comment