Mkurugenzi
Mkuu-Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu, Dkt Hassan Abbas amesem
kwamba Tundu Lissu bado ni mgonjwa na yuko wodini hivyo Serikali haioni
busara kulumbana naye kwa sasa.
Dkt Abbasi ameeleza kuwa, kwa sasa serikali bado inaendelea kumuombea mbunge huyo ili aweze kupona haraka.
Maneno
hayo yametolewa ikiwa ni mida mfupi tangu Tundu Lissu ambaye ni Mbunge
wa Singida Mashariki alipozungumza na waandushi wa habari akiwa
Hospitalini jijini Nairobi na kuituhuma serikali kuhusu masuala
mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Miongoni
mwa mambo mengi ambayo Tundu Lissu ameituhumu serikali ni pamoja na
jaribio la kutaka kumuua lililotokea Septemba 7 mjini Dodoma, ambapo
Lissu amesema licha ya kuwa miezi minne imepita tangu aliposhambuliwa
kwa lengo la kuuawa, hakuna kiongozi yoyote wa serikali aliyekemea tukio
hilo.
Lissu
ameelekeza malalamiko yake pia kwa Bunge ambapo amekosoa uamuzi wa
Bunge kukataa kugharamia matibabu yake, na kuacha mzigo wote kwa chama
na familia.
0 comments:
Post a Comment