Leo
January 5, 2017 Mfanyabiashara James Rugemarila anayekabiliwa na kesi
ya utakatishaji fedha amewataja wezi wa fedha za Escrow katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Kisutu kama alivyodai awali kuwa atawataja.
Wezi
hao amewataja mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba baada ya
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai kueleza upelelezi wa kesi
hiyo haujakamilika, hivyo anaomba iahirishwe hadi tarehe nyingine.
“Mwizi
ni Standard Chartered Tanzania Ltd na Standard Chartered Hong Kong
ambao wameisababishia serikali hasara ya Trilioni 37, pia nimewapelekea
TAKUKURU washiriki wengine wa fedha hizo, hivyo ninaomba niendelee kuwa
hai ili nije kuwa shahidi mzuri wa upande wa mashtaka kuhusu wezi hao.” –
James Rugemarila
Pia
Rugemarila amedai kuwa wezi hao ndio wamemuibia hata kwenye kampuni
anayoisimamia ya VIP ambayo inawadai Trillion 16. Wakili Swai alidai
kuwa ni kweli Rugemarila aliwasilisha taarifa ofisini kwao na
wanazifanyia kazi kisha watatoa majibu.
Tofauti
na hayo Rugemarila pia ameiomba mahakama imkubalie akafanyiwe uchunguzi
nchini India kwa sababu anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani kwa miaka 9
sasa huku mshtakiwa mwingine ambaye ni mmiliki wa IPTL Harbinder Singh
Sethi aliiambia Mahakama kuwa tatizo lake la ugonjwa linajulikana.
Kutokana
na hatua, Hakimu Simba amesema afya za washtakiwa ni muhimu hivyo
wafanyiwe uchunguzi, pia anautaka upande wa mashtaka ukamilishe
upelelezi kwa wakati, ambapo ameahirisha kesi hiyo hadi January 19,2018.
0 comments:
Post a Comment