Aliyekuwa
Waziri Mkuu wa Tanzania, Edward Lowassa, ametuma salamu za mwaka mpya
kwa Watanzania, akiwasihi kuwa, wakati wanaposherehekea mwaka mpya
wasikubali kugawanywa.
Lowassa
ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na
Maendeleo, (CHADEMA) amesema kuwa amani na mshikamano nndio nguzo muhimu
kwa Watanzania.
“Tunapouanza mwaka huu mpya, niwaombe watanzania wenzangu tukatae kugawanywa kwa sababu yoyote ile.
Umoja na mshikamano ndio nguzo yetu.”
Kwa
siku za hivi karibuni, Lowassa ambaye ni miongoni mwa wanasiasa
wakongwe nchini, amekuwa kimya, bila kuzungumzia masuala mbalimbali
yanayoibuka katika siasa za Tanzania.
0 comments:
Post a Comment