Mbunge
wa Kawe, Halima James Mdee amewataka watanzania kutumia mwaka mpya wa
2018 kutafakari kwa kina mwelekeo wa Tanzania na kuchukua hatua pale
panapohitaji kurekebishwa.
Mh.
Mdee ameyasema hayo kwenye salamu za Mwaka Mpya alizozitoa kupitia
mtandao wake wa kijamii ambapo amesema kwamba hakuna mwenye wajibu wa
ziada bali watanzania.
"Heri
ya Mwaka Mpya Watanzania we zangu. Mwaka 2018 tuutumie vyema kutafakari
kwa kina mwelekeo wa Taifa letu na tuchukue hatua kila mmoja kwa nafasi
yake pale ambapo tunadhani panahitaji kurekebishwa kwa maslahi mapana
ya nchi yetu. Hakuna mwenye wajibu wa ziada , Tanzania ni yetu!" Halima
Mdee.
0 comments:
Post a Comment