Baada
ya Mwenyekiti wa Bodi ya Parole nchini, Mh. Agustino Lyatonga Mrema
kusema anaenda kufungua kesi ya madai ya mabilioni ya shilingi TCRA kwa
watu waliomzushia taarifa za kifo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
imemuelekeza kiongozi huyo kuanzia kituo cha polisi kabla ya kufika
kwenye ngazi hiyo.
Akizungumza
baada ya Mrema kuwasilisha malalamiko yake katika Mamlaka hiyo Naibu
Mkurugenzi - Huduma za Bidhaa na Mawasiliano Bw. Tadayo Joseph amesema
kuwa Kabla ya Mrema kufika katika mamlaka hiyo alitakiwa kuanzia ndani
ya jeshi la polisi kwani malalamiko hayo yanahusu kosa la jinai.
"Mzee
Mrema na wananchi wengine wanaoleta taarifa za malalmiko tunawapongeza
kwa hatua hiyo. Suala ambalo alilileta ni linahusu kosa la jinai.
Mamlaka hii na jeshi la polisi zinafanya kazi kwa ukaribu sana.
Ameshauriwa kwanza akaripoti huko kisha atapatiwa wapelelezi kabla ya
kufika kwenye mamlaka hii,".
Mrema
ambaye alizushiwa kifo na watu wasofahamika siku ya Jumanne, aliahidi
jana kwenye kipindi cha East Africa Breakfast kwamba angekwenda
kufungua kesi TCRA na kisha kudai Bilioni 20 kutokana na matatizo pamoja na usumbufu uliosababishwa na mzushaji wa taarifa hizo.
Mbali
na hayo Mheshimiwa Mrema jana alisema alisema kitendo cha kuzushiwa
kifo kilimsaidia kujua ni watu gani wanampenda kweli na kina nani
hawampendi, kutokana na reaction zao baada ya taarifa feki za kifo
chake.
0 comments:
Post a Comment