Waziri
wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi amewataka viongozi wa
dini nchini kutimiza wajibu wao na kuhakikisha wanahifadhi vyema mapato
ya fedha na kuyaweka wazi kwa waumini ili kuondokana na migogoro
isiyokuwa ya lazima kwenye nyumba za ibada.
Aliyasema
hayo jana alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa katika Kanisa la Anglikana, Dayosisi ya Shinyanga kwenye ibada
ya kumuweka wakfu na kitini askofu wa pili wa dayosisi hiyo Johnson
Chinyong’ole ambaye alikuwa Katibu Mkuu wa Kanisa la Angilikana nchini
kisha mwaka jana kupendekezwa kuwa askofu.
Kabudi
aliwataka viongozi wa dini kutimiza wajibu wao na kuhakikisha
wanahifadhi vizuri mapato ya fedha kwa kuhakikisha yanaonekana kwa
waumini ili kuondokana na migogoro inayoibuliwa ndani ya nyumba za ibada
ikihusishwa na vitendo vya rushwa na ufisadi.
“Tunatambua
Kanisa la Angilikana limekuwa mstari wa mbele katika kutoa huduma za
kijamii kama maji, elimu na afya pale ambapo serikali imekwama
kupafikia. Dayosisi hii ni yenu wala siyo ya wazungu hivyo ni wajibu
kwenu kuhakikisha mapato ya fedha anaonekana ili kuondoa migogoro
isiyokuwa ya lazima kati ya viongozi na waumini,” alisema Waziri Kabudi.
Aliongeza:
“Serikali haina dini lakini ni wajibu wa kila Mtanzania kuwa na dini
yake hivyo viongozi wa dini wanatakiwa kuwa kiungo kati ya waumini na
askofu ikiwa kuwakumbusha kupiga vita rushwa, vitendo vya kishirikina na
ufisadi ambao serikali ya Rais Dk John Magufuli imekuwa ikipiga vita
kila siku”.
Pia
alitoa rai kwa askofu aliyewekwa wakfu na kitini, Chinyong’ole kuwa
awakumbushe waumini maadili ya kanisa katika kuwajenga kiroho na
kiuchumi lakini pia kutumia uongozi wake kuwajenga waamini ili waweze
kushirikiana kwenye mipango mbalimbali ya maendeleo.
Naye
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya utumishi wa Umma na
Utawala Bora, George Mkuchika ambaye ni mlezi wa kanisa hilo alisema
kuwa kanisa hilo limepitia wakati mgumu kwani kulikuwa na vuguvugu la
migogoro kwa baadhi ya waumini kujidai wanazishika nyadhifa ambazo
kuzipata zimeonekana kumbe kunautaratibu wake hivyo kushikamana na kwa
umoja na kuepuka migogoro.
Askofu
Mkuu wa kanisa hilo nchini, Jacob Chimeledya alisema kuwa kuna kazi
kubwa na kwamba hali iliyopo ni mapito hivyo aliiomba serikali
kulisimamia kanisa hilo kiuchumi kwani tayari limeanza mchakato wa
kuanzisha chombo chake cha kusimamia na kuliangalia mali zake.
0 comments:
Post a Comment