Ujio wa albam mpya yenye Jina la Shukrani ya mwanamziki nguli wa Injili nchini Tanzania Goodluck Gozbert umezua gumzo kwa watanzania hususani wa nyanda za juu kusini alipokuwa akizungumzia ujio wa albam hiyo kupitia kituo cha Redio kitulo fm kilichopo wilayani makete mkoani njombe.
Goodluck amesema ujio wa
albamu ya shukrani umetokana na mafanikio makubwa aliyoyapata katika albam yake
ya Ipo siku,hata hivyo ameongeza kusema pamoja na tuzo mbalimbali alizopata
kupitia muziki Bado anaamini Pasipo msaada wa Mungu asinge weza.
Aidha goodluck gozbert
ametoa wito kwa watanzania kuendelea kutoa sapoti kwa waimbaji katika kazi zao
huku akiweka bayana kuwa sasa albam ya shukrani yenye jumla ya nyimbo nane ipo madukani.
Nizaidi ya miaka miwili sasa
mwimbaji huyu wa nyimbo za Injili ameendelea kuteka soko la muziki wa kupitia
muziki unaotambulika kama Gospelfreva,na kupitia muziki wake waimbajiwengi
wamejikuta wanaiga muziki huo .
swali Je,wanaweza kutusua?
Tizama video hii kupitia
AFRICANI NEWS BLOG.
......................
0 comments:
Post a Comment