Mwanamuziki
wa Nyimbo za Injili nchini Tanzania Matha Baraka atoa siri nzito ya
kufanikiwa kimuziki huku akitoa wito kwa waimbaji wa nyimbo za Injili
kumtumikia Mungu kwa waminifu hali wakijua kuwa waimbaji wana hubiri
Neno kupitia Wimbaji.
Matha Baraka amesema kuwa
siri kubwa ni wokovu na kuishi kwa kumtegemea Mungu,ameyasema hayo alipokuwa
akizungumza na AFRICAN NEWS BLOG huku akisema mafanikio hayo yametokana na
kumtumikia Mungu kwa waminifu na bidii.
Aidha amesema kwa mwaka 2018
amejipanga zaidi katika kufanya Injili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania
ambapo amesema kwa mwaka 2017 amemwona Mungu akimtumia katika viwango Vya juu
zaidi ambapo muda mwingi amekuwa akihudumia maelfu ya watu katika maeneo tofauti.
Katika hatua nyingine Bi, Matha
Baraka,ametoa wito kwa waimbaji kutoimba kwa mazoeya na kuimba kwa kusikia
sauti ya kristo kuliko kuiga mafuta (uimbaji) ya wengine ambapo amesema kila
mwimbaji ana ujumbe ambao Mungu amempa kwaajili ya watu wake.
Kwa sasa Matha Baraka anatamba
na Albamu ya Nimekuja na Maua una weza kuitazama kupitia Yotube,na mitandao
mingine ya kijamii.
0 comments:
Post a Comment