Ngili
wa muziki wa dansi, Nguza Vicking ‘Babu Seya’ na mwanaye Jonhson Nguza
‘Papii Kocha’ kwa mara ya kwanza tangu waachiwe huru Desemba 9 kwa
msamaha wa Rais John Maguuli, leo Januari 5 wamekutana na Naibu Waziri
wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Juliana Shonza pamoja na
wanahabari ambapo wamepata fursa ya kueleza namna walivyojipanga kurudi
kwenye tasnia ya muziki.
Akizungumza
na wanahabari katika Studio za Wanene Entertainment zilizopo Mwenge,
Coca-cola, Naibu Waziri Shonza amesema wao kama wizara kazi yao kubwa ni
kuwasaidia wasanii na kuhakikisha wanafanikiwa kufikia malengo yao,
hivyo wameamua kuwakutanisha na wadau wa muziki wakiwemo Wanene ili
kufanmikisha zoezi la nguli hao kurudi kwenye game.
“Sisi
kama wizara kuna namna ambayo tunaitumia kuwasapoti wasanii, hatuwezi
kutoa fedha, hivyo tumeamua kuwakutanisha Babu Seya, Papii Kocha na
Studio ya Wanene ili waweze kuweka mipango sawa kwa ajiri ya kuendeleza
muziki,” alisema Shonza.
Kwa
upande wake Babu Seya alisema mashabiki wao watulie kwani mipango ndiyo
inapikwa hivyo mambo yakikamilika kila kitu watakiweka hadharani.
“Baada
ya shooting na recording tutaangalia namna ya kufanya lakini hatutakuwa
na utaratibu wetu wa zamani wa kupiga shoo kila siku,” alisema Babu
Seya huku papii Kocha akiachia kionjo cha moja ya wimbo wao wa zamani.
Aidha,
Mmiliki wa Studio za Wanene, Dash alisema wao wamejipanga kutoa sapoti
ya ainza zote kwa babu Seya na papii ili kuhakikisha wanarekodi kazi
nzuri na kuzifikisha kwa jamii na mashabiki wao.
0 comments:
Post a Comment