Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda jana ametembelea na kutoa
pole kwa Familia ya Wastaafu ya Bwana Edward Bejumula na Bi. Stella
Bejumula walioteseka kwa Miaka Sita bila Makazi baada ya kudhulumiwa
Nyumba yao ambapo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kuhakikisha haki
inatendeka bila kuvunja sheria.
RC
Makonda amewatembelea wastaafu hao na kuwapatia Masada wa vitu
mbalimbali ikiwemo Mchele, Unga, Sabuni, Ngano, Mafuta,Nyama,Viazi,
Maharage, Sukari, Vitunguu, Ndizi, Nyanya kwaajili ya matumizi ya
nyumbani baada ya familia hiyo kupoteza Mali zote.
Story
ya wastaafu hao kudhulumiwa Nyumba waliyojenga baada ya kufanya kazi
kwa Miaka 34 imemgusa RC Makonda hadi kujikuta anashindwa kuvumilia na
kutokwa na machozi kutokana na namna inavyohuzunisha kuona mnyonge
anajituma kwenye kazi na kufanikiwa kujenga nyumba alafu anatokea mtu
anamdhulumu Mali yake.
Makonda
amesema kazi ya kutafuta haki ya wastaafu hao inaanza Mara moja kwa
kuwahoji watu wote waliohusika na sakata hilo wakiwemo Bank, Muuzaji wa
nyumba, Mnunuzi, kampuni ya udalali ya Majembe, Watu wa Mahakama na watu
wa ardhi.
Kwa
sasa wastaafu hao wanaishi kwenye nyumba ya mfadhili mmoja aliejitolea
kusitiri familia hiyo ambapo RC Makonda amemshukuru kwa moyo
alioonyesha.
Kwa
upande wao Wastaafu waliodhulumiwa Mali zao wamefurahia kitendo cha RC
Makonda kuona taarifa zao kwenye vyombo vya habari kisha kuwatembelea na
kuwasikiliza kitendo kilichowafariji na wanaamini kwa utendajikazi wa
RC Makonda wanapata haki yao.
Aidha
wamemshukuru RC Makonda kwa kitendo cha kuwapelekea Chakula kwakuwa
wameishi maisha ya tabu hadi kukosa vitu vya ndani ikiwemo vyakula
ambapo wamemuombea kwa Mungu azidi kumpa maarifa ya kuwasaidia wananchi
wanyonge.
0 comments:
Post a Comment