Mbunge
wa Chalinze kupitia Chama cha Mpainduzi (CCM), Ridhiwani Kikwete
amekanusha ujumbe unaosambazwa katika mitandao ya kijamii ukidai kuwa
amekikosoa chama hicho kutokana na kutoridhishwa na mwenendo wake.
Akizungumza
jana jioni, Ridhiwani amewataka watanzania na wanachama wa CCM kupuuza
taarifa hiyo kwani siyo yeye ameitoa na badala yake ni watu wenye lengo
lakukiharibu chama hicho.
Amesema
kwamba, kwa siku nzima ya jana hajaandika ujumbe wowote na kwamba
alikuwa jimbo kwake katika vikao vya halmashauri wakipanga mipango ya
bajeti kwa ajili ya maendeleo ya jimbo hilo.
Msikilize Ridhiwani hapa chini;
0 comments:
Post a Comment