Home » » LHRC yatoa kauli kuadhibiwa vituo vya televisheniLHRC yatoa kauli kuadhibiwa vituo vya televisheni

LHRC yatoa kauli kuadhibiwa vituo vya televisheniLHRC yatoa kauli kuadhibiwa vituo vya televisheni

Unknown | Wednesday, January 03, 2018 | 0 comments
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimeviomba vyombo vya kimataifa vinavyohusika na uangalizi wa haki za binadamu kuingilia kati suala la uhuru wa kujieleza nchini.

LHRC pia imetaka Serikali kuheshimu Katiba kwa kutoingilia uhuru wa kujieleza.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumatano Januari 3,2018 siku moja baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuvitoza faini vituo vya televisheni vya ITV, Azam Two, Startv, Channel Ten na EATV kwa kukiuka kanuni ya maudhui ya mwaka 2005.

Mkurugenzi Mtendaji wa LHRC, Dk Hellen Kijo-Bisimba amesema uamuzi wa kutozwa faini vituo hivyo ni ukandamizaji wa uhuru wa vyombo vya habari wa kutoa taarifa kwa jamii na hasa zinazoikosoa Serikali.

"Serikali ikubali kuyasikiliza mazuri na mabaya na kuyatumia maoni ya wananchi. Vituo hivi vimetozwa faini kwa sababu vimetoa taarifa ya tathmini iliyotolewa na LHRC kuhusu uchaguzi mdogo wa madiwani uliofanyika Novemba mwaka jana,” amesema.

Dk Kijo –Bisimba amesema, "Kwetu  tunaona hili si sawa na tunaona mambo haya yanazidi kuongezeka, Serikali kupitia Jeshi la Polisi wamekuwa wakitumia neno uchochezi kuminya uhuru wa mawazo na kujieleza."

Amesema kutokana na hilo, LHRC ipo tayari kuungana na wadau ambao wako tayari kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya neno uchochezi na baadhi ya vifungu vya kanuni ya maudhui.

Dk Kijo -Bisimba amesema LHRC imeanzisha harambee kuchangia gharama kuvisaidia vyombo vya habari vilivyokumbwa na adhabu hiyo.

Advertisement
==

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG