MAPATO
kutokana na mauzo ya korosho katika msimu wa 2017/2018 katika mikoa
minne ya Lindi, Mtwara, Pwani na Ruvuma yamepanda na kufikia sh.
trilioni 1.08 ikilinganishwa na misimu miwili iliyopita.
Kaimu
Mkurugenzi wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Bw. Hassan Jarufu alitoa
taarifa hiyo Jumapili, Desemba 31, 2017 wakati akitoa ufafanuzi juu ya
uzalishaji na mauzo ya zao la korosho nchini hadi kufikia mwisho wa
mwaka 2017.
“Ukiangalia
msimu wa mwaka 2015/2016, utaona kuwa korosho zilizozalishwa zilikuwa
kidogo zaidi. Msimu huo ziliuzwa kilo 155,244,645 zikiwa na thamani ya
sh. 388,474,530,906.00 ikilinganisha na msimu wa 2016/2017 ambapo jumla
ya kilo 265,237,845.00 ziliuzwa zikiwa na thamani ya sh.
871,462,989,284.00,” alisema.
Alisema
katika minada 10 ya msimu wa 2017/2018, mauzo ya korosho yamefikia kilo
285,828,205 zenye thamani ya sh. 1,082,200,383,581.00. “Mnada wa 10
ulikuwa tarehe 21 Desemba, 2017 na minada bado inaendelea kwa msimu wa
2017/2018,” alisema.
Akitoa
ufafanuzi wa mauzo hayo kwa kila mikoa hadi kufikia mnada wa 10, Bw.
Jarufu alisema Mkoa wa Mtwara umeongoza kwa kuuza tani 178,165.741 zenye
thamani ya sh. 701,674,466,366.00 ukifuatiwa na mkoa wa Lindi ambao
umeuza tani 68,687.504 zenye thamani ya sh. 247,163,294,296.00.
“Mkoa
wa Ruvuma umeuza tani 19,545.613 zenye thamani ya sh. 76,173,400,063.00
na mkoa wa Pwani umeuza tani 19,429.347 zenye thamani ya sh.
57,189,224,856.00 na kufanya mapato yote kwa mwaka huu kufikia sh.
trilioni 1.082,” alisema.
Bw.
Jarufu alitoa ufafanuzi huo mara baada ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kuzindua kampeni ya kitaifa ya upandaji mikorosho bora na mipya milioni
10 kwa msimu wa 2017/2018 mjini Ruangwa, mkoani Lindi. Kaulimbiu ya
kampeni hiyo ni: “Korosho ni dhahabu ya kijani, tuitunze, itutunze”.
Bw.
Jarufu alimweleza Waziri Mkuu kwamba Bodi ya Korosho Tanzania kwa
kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele, Sekretarieti za
Mikoa na Halmashauri za wilaya, imeendelea kutekeleza mpango wa miaka
mitatu wa kupanda mikorosho 10,000,000 kila mwaka.
“Katika
mpango huu, wastani wa mikorosho 5,000 inatarajiwa kupandwa katika kila
kijiji au mikorosho 30 kwa kaya kwa mwaka, sawa na ekari 330,000 kwa
mwaka kwa nchi mzima. Lengo la mpango huu ni kuongeza kiasi cha korosho
kinachozalishwa nchini kwa kuongeza wigo wa halmashauri zinazozalisha
korosho na kupanda miche inayotokana na mbegu bora zenye uzalishaji
mkubwa na zenye ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu,” alisema.
Alisema
katika msimu wa 2017/2018, Bodi ya korosho inaratibu uzalishaji wa
jumla ya miche 14,001,820 ambayo imetokana na tani 100 (kilo100, 000)
zilizozalishwa na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Naliendele.
“Mchanganuo
wake ni kama ifuatavyo: kilo 31,170 za mbegu zitapandwa shambani moja
kwa moja ambazo zitatoa jumla ya miche 2,181,900; kilo 68,830
zitazalisha jumla ya miche 11,819,920 kati ya miche hiyo isiyobebeshwa
ni 9,636,200 na miche itakayobebeshwa ni 2,183,720.
“Ni
matumaini yetu kuwa ifikapo mwishoni mwa mwezi Februari 2018, miche
yote itakuwa tayari imezalishwa, kugawanywa na kupandwa katika mashamba
ya wakulima,” aliongeza.
Mkurugenzi
huyo alisema, katika msimu huu eneo la utekelezaji wa mradi
limeongezeka kutoka Halmashauri 51 za msimu uliopita 2016/2017 hadi
kufikia Halmashauri 90 nchi nzima ikiwemo mikoa mipya iliyothibitishwa
kustawi zao la korosho hapa nchini.
Sherehe
hizo zilihudhuriwa na wakuu wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvuma, Pwani na
wajumbe wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT). Wakuu wa Wilaya, baadhi ya
Wenyeviti wa Halmashauri na wataalamu kutoka kituo cha utafiti cha
Naliendele walishiriki uzinduzi huo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
0 comments:
Post a Comment