HATIMA
ya mafao ya wafanyakazi wa serikali walioondolewa kwenye ajira kutokana
na kubainika kuwa na vyeti feki itajulikana kabla ya Bunge la Bajeti,
imefahamika.
Hatua
hiyo inatokana na serikali kujibu hoja nane za Shirikisho la Vyama vya
Wafanyakazi Tanzania (Tucta) na kwamba suala la kulipwa au kutolipwa
haki zao litafahamika Machi au Aprili, mwaka huu.
Hoja
zingine ni ajira ya waliomaliza darasa la saba, kupandishwa madaraja,
madeni ya wafanyakazi, nyongeza za mishahara, kutofanyika vikao vya
bodi, kujua idadi ya taasisi zilizoundwa na kuunganishwa kwa Mifuko ya
Hifadhi ya Jamii.
Katibu
Mkuu wa Tucta, Dk. Yahya Msigwa, alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa
mamlaka mbalimbali zinamalizia kulifanyia kazi suala la vyeti feki na
kwamba kabla ya Mei Mosi, mwaka huu, hatima yao itakuwa imepatikana.
“Unajua
kilichofanyika ni kosa la jinai na la kinidhamu, hivyo sisi Tucta
tunaendelea kuiomba serikali angalau wapatiwe kifuta machozi,” alisema.
Alisema
ajira kwa waliomaliza darasa la saba Serikali ilitoa waraka unaosema
watumishi wa umma wanapaswa kumaliza elimu ya kidato cha nne kuanzia
Mei, 20, 2004.
Pia
alisema baada ya hapo, walitakiwa kujiendeleza ili kuwa na vigezo vya
kuendelea kuwa watumishi wa umma iwapo zipo baadhi ya idara zinawahitaji
na kujenga hoja.
Kuhusu kupandishwa madaraja,
Dk.
Msigwa alisema watumishi wengi hawajapandishwa kutokana na uhakiki wa
vyeti, hivyo serikali imetenga fedha kwa ajili ya mpango huo kwa
kutegemea bajeti ijayo.
Alisema
malipo yataanza tangu siku ya kupata barua ili kupunguza madeni ambayo
inadaiwa na kwamba kimsingi katika hilo, yako madeni ya mishahara na
isiyo ya mishahara.
Kuhusu
madeni, kwa mujibu wa Dk. Msigwa, serikali imesema imemaliza uhakiki na
imeanza kulipa lakini itakuwa vigumu kulipa watu wote kwa mkupuo bali
watazingatia uhakiki ya madeni yenyewe.
Kwa
upande wa nyongeza ya mishahara, alisema Rais John Magufuli hakuahidi
wakati wa sherehe za Mei Mosi bali nyongeza hiyo italolewa mwaka huu.
Aidha,
Dk. Msigwa alisema hoja ya kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii
kuwa na mifuko miwili, mmoja wa binafsi na mwingine wa umma, imetokana
kauli za wafanyakazi wenyewe kwenye sherere za Mei Mosi.
Alisema rasimu iliyotegenezwa si mbaya licha upungufu uliopo na wanaendelea kutoa maoni kabla muswada haujawasilishwa Bungeni.
0 comments:
Post a Comment