Diwani
wa Kata ya Namichiga kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), wilayani Ruangwa mkoani Lindi Bwana, Mikidadi Ibadi Mbute,
amejiuzulu nafasi yake na kutangaza kujiunga na CCM baada ya kuridhishwa
na kasi ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
Pia
Bakari Hamisi Mpanya maarufu kama Selenge aliyekuwa Diwani wa Kata ya
Nachingwea, kupitia Chama cha Wananchi (CUF), amejiunga na CCM na kusema
ameridhishwa na kasi ya mbunge wa Ruangwa na Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa.
0 comments:
Post a Comment