Home » » BREAKING: Rais Magufuli aongeza baraza la mawaziri. ........Amteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini

BREAKING: Rais Magufuli aongeza baraza la mawaziri. ........Amteua Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini

Unknown | Saturday, January 06, 2018 | 0 comments
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 06 Januari, 2018 amemteua Mhe. Doto Mashaka Biteko kuwa Naibu Waziri wa Madini.

Mhe. Doto Mashaka Biteko ni Mbunge wa Jimbo la Bukombe na  alikuwa Mwenyekiti wa kamati ya muda iliyochunguza madini ya Tanzanite.

Kufuatia uteuzi huu Wizara ya Madini sasa itakuwa na Waziri na Naibu Mawaziri wawili.

Mhe. Rais Magufuli amefanya uteuzi huu kwa lengo la kuongeza nguvu kutokana na uwingi wa majukumu katika Wizara ya Madini.

Mhe. Doto Mashaka Biteko ataapishwa Jumatatu tarehe 08 Januari, 2018 saa 3:00 asubuhi Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
06 Januari, 2018

Advertisement
==
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG