Mwanasiasa
mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru leo Jumamosi amepewa taarifa za
kifo cha mke wake Pares Mwiru ambazo imeelezwa kuwa amezipokea kwa
mshtuko mkubwa.
Kingunge
aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wodi ya Mwaisela
akipatiwa matibabu baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake
Kijitonyama, alifanyiwa upasuaji Januari 4 mwaka huu.
Leo Januari 6, mtoto wa mwanasiasa huyo Kinje Mwiru amesema wamempa taarifa baba yao saa tano asubuhi leo.
“Tumemfahamisha
leo saa tano, ilikuwa ni vigumu sana wakati tunamfikishia taarifa hizo
na amezipokea kwa ugumu sana. Haikuwa rahisi kwa yeye kupokea taarifa
wakati tunamweleza,” amesema.
Kinje amesema kwa sasa wamemuacha apumzike ili aweze kuwapatia mwongozo nini kifanyike baada ya kifo cha mke wake.
Pares
alifariki Januari 4 saa nane mchana katika wodi ya Sewahaji alikokuwa
amelazwa, tangu alipofikishwa Muhimbili Oktoba 3, mwaka jana.
Ofisa Uhusiano wa MNH John Stephen amesema kwa sasa afya yake imeimarika.
"Anaendelea
vizuri na afya yake imetengamaa, bado yupo chini ya uangalizi wa karibu
wa madaktari, baada ya upasuaji aliofanyiwa," amesema.
0 comments:
Post a Comment