Waziri
wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku kumi kwa jengo la Tanesco
lililopo Ubungo libomolewe ili kupisha ujenzi wa barabara ya Morogoro.
Waziri
huyo pia amewataka watumishi wa Tanesco wanaosimamia jengo hilo na
wakandarasi waliowekwa kubomoa jengo hilo wasisafiri wala kusherekea
Sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya bali washughulikie jengo hilo
kuvunjwa.
“Nataka
kuanzia leo Desemba 22 ndani ya siku sita jengo hili lote libomoke na
kwasababu ni majengo mawili ndani ya siku kumi majengo yote mawili yawe
yamebomoka kama mnaona vigumu kubomoa jengo lenu waambieni TBL ”amesema
Amesema
hadi kufikia mwisho wa mwezi huu jengo hilo lote liwe limeanguka chini
na hakuna cha sikukuu wala Krisimasi kwenye kubomoa jengo hili na ujenzi
wa barabara kama Tanesco wanaaza waanze tusiwakwamishe”amesema.
Amesema
wananchi wameshabomoa majengo yao kwanini Tanesco bado wanasuasua na
kudai Januari mosi ataenda tena kukagua kuona kama agizo lake
limefanyiwa kazi.
“Naimani
wananchi hawatapata shida wakati wa sikukuu ya Krismasi na mwaka mpya
,kwa hiyo asiruhusiwe mtumishi yoyote wa Tanesco kwenda nje ya ofisi
yake wakati wa sikukuu zote mbili”amesema
Hata
hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Kahitwa Bishaija amesema wamelisikia
agizo la Waziri na wataenda kulitekeleza kama lilivyo.
0 comments:
Post a Comment