Jeshi
la Polisi Mkoa wa Mtwara linamtafuta Zuhura Ismail Mkazi wa Halmashauri
ya Nanyamba Mkoani Mtwara kwa Kosa la Kumuua Aliyekuwa Mume wake kwa
Kuchoma nyumba waliyokuwa wakiishii kwa kutumia mafuta ya Petrol
kutokana na Wivu wa kimapenzi.
Zuhura ambaye anatafutwa na jeshi la Polisi,Majira ya Usiku alifika
Nyumbani kwa mume wake huyo ambaye walikuwa wametengana na Kuhisi kuwa
Ndani ya nyumba Mumewe alikuwa amelala na mwanamke Mwingine Hivyo
Kuchoma Nyumba Moto na Kutokomea Kusikojulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya amewaomba wananchii
wanamfahamu kutoa taarifa popote watakapomuoa Mwanamke Huyo Zuhura
Ismail.
Aidha kamanda Mkondya ameongeza kuwa Watu 12 wanashikiliwa na polisi kwa
tuhuma za Wizi wa pikipiki pamoja na Kuvunja nyumba za watu na kuiba
Vifaa mbalimbali vya majumbani.
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara Limewataka wananchi waliotoa
taarifa za kuibiwa wafike kituo cha Polisi kwa ajili ya Kutambua na
kuchukua mali zao.
Pichani.Kamanda
Wa Police Mkoa wa Mtwara Lucas Mkondya akiwaonesha waandishi wa Habari
(hawapo pichani) Samani za Ndani Zilizokamatwa baada ya Kufanya
Opereshen ya Msako kwa Watuhumiwa wa wizi pamoja na Madumu ya Pombe
haramu ya Gongo Lita 369 ambapo watu 15 wamekamatwa wakifanya Biashara
ya Kuuza na Kusafirisha.
0 comments:
Post a Comment