Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida Debora Magiligimba amesema Jeshi la Polisi
Mkoani kwake linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kukutwa na
madawa ya kulevya
Kamanda Magiligimba
amesema katika oparesheni ya kupambana na dawa za kulevya wamefanikiwa
kuwakamata watuhumiwa hao wakiwa na misokoto ya bangi 238 sawa na gramu
484 na kete 80 za Heroin sawa na gramu 160.
“Mbinu
zilizotumika kuhifadhi Heroin ni mtuhumiwa aliamua kuficha kete kwenye
matundu ya sabufa na kuanza kuuza kidogo kidogo na misokoto ya bangi
ilifichwa kwenye begi dogo la nguo na kupuliziwa marashi ili kuzia
harufu ya bangi.”,amesema Kamanda Magiligimba.
Kamanda Magiligimba amesema watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani mara baaada ya upelelezi kukamilika.
0 comments:
Post a Comment