Mwanafunzi
wa kidato cha pili katika shule ya sekondari Enhencement Center iliyopo
mkoani Njombe, aliyefahamika kwa jina moja la HOSSANA amefariki dunia
baada ya kupigwa na shoti ya umeme wakati akianika nguo kwenye kamba ya
waya.
Tukio
hilo limetokea mtaa wa Kambarage Mkoani Njombe ambapo kwa mujibu wa
shuhuda Daud Given Mwatija ambaye ni Afisa magereza amesema katika mtaa
wao ni kweli mwanafunzi huyo amefariki ambapo kulikuwa na waya
unaopeleka umeme kwenye jengo walilokuwa wakiishi (familia ya mwanafunzi
huyo) uliokuwa umechubuka na kugusa nyumba hiyo hali iliyopelekea jengo
zima kuwa na umeme, lakini wakati mwanafunzi huyo akianika nguo kwenye
kamba ya umeme hakujua kama waya huo nao ulikuwa ukipitisha umeme,
akapigwa shoti na kufariki dunia
Tukio hilo limetokea jana
0 comments:
Post a Comment