Mkurugenzi
mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Ndugu Francis Namaumbo amwewaomba
wananchi wilayani makete kujitokeza kupima maambikizi ya virusi vya Ukimwi ili
kupunguza ongezeko la maambukizi mapya ya VVU katika wilaya ya Makete mkoani Njombe.
Rai
hiyo ameitoa hapo jana katika Tamasha la
Nguvu ya Mwaka 2017 lililoandaliwa na kitulo Fm Radio ambalo lililofanyaka ukumbi wa madihani Villas Lodge.
Namaumbo
ameongeza kuwa kutokana na wilaya ya makete kuwa na ongezeko kubwa la virusi
vya ukimmwi amewaomba vijana pamoja na wananchi kwa ujumla kujitokeza kupima
ili kujua afya zao.
Mkurugenzi
wa Madihani Villas Lodge Abel Mbilinyi ameipongeza Kitulo Fm Redio kwa kuandaa
Tamasha hilo la kutoa Elimu kwa Vijana kuhusu Fursa mbalimbali za kiuchumi na
Wadau wote waliofika Ukumbini hapo
Kitulo
fm Radio iliandaa Tamasha la nguvu ya mwaka 2017 kwa lengo la kupunguza
maambukizi ya virusi vya ukimwi,kutoa elimu kwa vijana kuhusu fursa za
ujasiriamali,kutoa elimu kwa wananchi kuhusu ukatili kwa watoto,kutoa elimu kuhusu
kutokomeza rushwa katika wilaya ya makete.
Mratibu
wa Tamasha la nguvu ya mwaka Aldo sanga kwa kushirikiana wafanya kazi wa kitulo
fm radio wamewashukuru wadau wote waliohudhurua kwenye tamasha hilo.
0 comments:
Post a Comment