Home » » Tuache kulalamika 2018 - Dewji

Tuache kulalamika 2018 - Dewji

Unknown | Thursday, December 28, 2017 | 0 comments
Bilionea anayemiliki kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises nchini (MeTL), Mohammed Dewji `Mo' amefunguka na kutoa ujumbe wake kwa vijana kuelekea mwaka 2018 na kuwataka vijana na Watanzania kiujumla kuacha kulalamika mwaka 2018

Dewji katika ujumbe wake huo alioutoa kupitia mitandao yake ya kijamii amewashi Watanzania kama wanaona hawapendezwi na kitu fulani njia nzuri ni kukibadili kitu hicho na kuacha kulalamika kwani hakutaweza kubadili jambo lolote lile. 
"Kama hupendi kitu fulani, (jaribu) kibadilishe! Unataka kupunguza uzito? Badilisha milo yako, fanya mazoezi. Unataka kukutana na watu wapya? Toka nje, tembea na jichanganye na watu wengine! Kumbuka kulalamika hakubadilishi jambo usilolipenda!" alisisitiza Dewji
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG