Licha
ya kutokiri moja kwa moja juu ya taarifa zinazosambaa mitandaoni kuhusu
kumkamata Askofu Zakaria Kakobe wa Kanisa la Full Gospel Bible
Fellowship (FGFC) lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam, Jeshi la Polisi
limesema ni lazima litamhoji kiongozi huyo wa kiroho.
Kuhojiwa huko kumetokana na kauli yake dhidi ya serikali aliyoitoa wakati wa ibada ya Krismasi.
Jana,
kulienea taarifa kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kueleza kwamba
askofu huyo alitiwa mbaroni jana asubuhi na askari wa Jeshi la Polisi
huku sababu za kukamatwa zikielezwa kuwa ni ujumbe alioutoa wakati wa
mahubiri yake ya ibada ya Krismasi.
Akizungumza
na Nipashe jana kuhusiana na ukweli wa taarifa za kutiwa mbaroni kwa
Askofu Kakobe, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro
Mambosasa, alisema kuwa ni kweli walishakuwa katika harakati za
kumkamata.
"Ametoa maneno ya kashfa katika mahubiri yake, lakini sina taarifa kama amekamatwa," Kamanda Mambosasa alisema na kuongeza:
"Taarifa za kumkamata zipo, lazima tumkamate. Tutamhoji…tutamhoji alikuwa na maana gani.
“Mtu akitenda kosa la jinai ni lazima akamatwe…kwa sasa niko msibani, sijapokea taarifa kama amekamatwa au kuhojiwa. Nitawaarifu kama kutakuwa na taarifa zaidi.”
“Mtu akitenda kosa la jinai ni lazima akamatwe…kwa sasa niko msibani, sijapokea taarifa kama amekamatwa au kuhojiwa. Nitawaarifu kama kutakuwa na taarifa zaidi.”
Askofu
Kakobe (62), anadaiwa kuyatumia mahubiri yake siku hiyo kuzungumzia
mwenendo wa serikali na masuala mbalimbali ya kisiasa nchini.
Mojawapo
ya sauti inayodaiwa kuwa ya Askofu Kakobe na kusambaa kwenye mitandao
ya kijamii ilidai kwamba hivi sasa Tanzania si nchi ya chama kimoja kama
viongozi wanavyotaka.
Chanzo: Nipashe
0 comments:
Post a Comment