Jeshi
la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro linamshikilia mfanyakazi wa kike wa
Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) kwa tuhuma za kukutwa na
dawa za kulevya aina ya bangi ndani ya gari lake.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issa, amesema kwamba mtuhumiwa
huyo ambaye ni mkazi wa Karanga katika Halmashauri ya Manisapaa ya
Moshi, alikamatwa akiwa na kilogramu 216.3 za bangi ndani ya gari lake
aina ya Toyota Sienta.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa eneo la Majengo kwa Mtei, Disemba 19 alipokuwa njiani akitokea Himo.
Kamanda
Issa amesema kuwa, biashara ya bangi inabaki kuwa changamoto kubwa sana
katika mikoa ya kaskazini, na kwamba jeshi la polisi linafanyakazi kwa
jitihada zote kuhakikisha linatokomeza hali hiyo.
Aidha,
alionesha masikitiko yake kufuatia watumishi wa umma ambao ndio
walitakiwa kuwa mstari wa mbele kupiga vita dawa za kulevya,
wakijihusisha kwenye biashara hiyo.
0 comments:
Post a Comment