Kufuatia
sakata la umiliki wa kampuni ya mawasiliano ya Airtel, Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) Disemba 28, 2017 iliziandikia benki zote na taasisi za
kifedha ambazo zimekuwa zikisimamia akaunti za iliyokuwa Celtel, Zain au
Airtel kuwasilisha taarifa hizo.
BoT imezitaka taasisi hizo ama benki kueleza kama zimewahi kuendesha ama zinaendesha akaunti zinazohusiana na kampuni tajwa.
Aidha,
taasisi zote ambazo zitakuwa zina akaunti za kampuni hiyo tajwa,
zimetakiwa kuwasilisha jina la akaunti, namba ya akaunti, aina ya fedha
zilizomo kwenye akaunti na kiwango cha mwisho kilichokuwemo kwenye
akaunti hadi Disemba 27, 2017.
Taarifa za akaunti hizo zinazotakiwa kuwasilishwa ni kaunzia Januari 1, 2000 hadi Disemba 27, 2017.
Taarifa
zinazotakiwa kuwasilisha zinatakiwa kuwa katika nakala ngumu (hardcopy)
na nakala teke (soft copy) na zilitakiwa kuwasilishwa jana saa 5
asubuhi.
0 comments:
Post a Comment