Marekani imewawekea vikwazo maafisa wawili wa Korea Kaskazini ambao inasema kuwa wamechangia kuundwa makombora ya nchi hiyo.
Wizara
ya fedha nchini Marekani iliwataja Kim Jong-sik na Ri Pyong-chol na
kusema kuwa wote walikuwa viongozi wakuu katika mpango wa makombora ya
masafa marefu wa Korea Kaskazini.
Baraza
la ulianzi la Umoja wa Mataifa liliiwekea vikwazo vipya Korea Kaskazini
siku ya Ijumaa kujibu majaribio yake ya makombora ya masafa marefu.
Korea Kaskazini ilisema kwa hatua hiyo ni kama ya vita.
Vikwazo
hivyo vipya vya Marekani vitazuia shughuli zozote za wanaume hao wawili
zinazofanywa nchini Marekani, na hata kutwaliwa kwa mali zao zilizo
nchini Marekani.
Wanaume
hao wawili wanaonekana mara kwa mara wakiwa na kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-un wakiwa maeneo ya kuyafanyia majaribio makombora.
Mwaka huu nchi hiyo imefanya majaribio kadha ya makombora tofauti ambayo inasema kuwa yanaweza kufika nchini Marekani.
0 comments:
Post a Comment