Aliyekuwa nyota wa soka, George Weah, ametangazwa mshindi wa uchaguzi wa marudio wa urais uliofanyika nchini Liberia.
Tume
ya uchaguzi ya nchi hiyo ilisema kwamba Weah alipata asili mia 61.5 ya
kura zote zilizopigwa na kupata ushindi kwenye kaunti 14 kati ya 15.
Weah,
mwenye umri wa miaka 51, alikuwa anashindana na makamu wa rais Joseph
Boakai, kila mmoja akitaka kujaza nafasi ya rais Ellen Johnson Sirleaf,
ambaye anaondoka mamlakani baada ya mihula miwili inayoruhusiwa na
katiba ya Liberia.
Sirleaf
alimshinda Weah kwenye uchaguzi wa mwaka 2005, baada ya nchi hiyo ya
Afrika Magharibi kuibuka kutoka kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Tume
ya uchaguzi ilisema asilimia 56 ya wapiga kura walijitokeza, ambao ni
wachache kuliko waliojitokeza tarehe 10 mwezi Oktoba, wakati wa duru ya
kwanza ya uchaguzi huo.
Waangalizi walisema kwamba vituo vya kupigia kura wiki hii vilikuwa na utaratibu mzuri kuliko uchaguzi wa oktoba.
Mgombea
mwenza wa Weah, Jewel Howard Taylor, ni mke wa zamani wa aliyekuwa rais
wa Liberia Charles Taylor, aliyeanzisha vita vya wenyewe kwa wenyewe
nchini humo na ambaye anatumikia kifungo cha miaka 50 nchini Uingereza
kwa majukumu yake katika ukatili uliotokea nchini Sierra Leone.
Weah alikuwa mwanasoka mwenye umaarufu mkubwa mnamo miaka ya 90. Alichezea timu kama vile Chelsea, Manchester City na AC milan.
0 comments:
Post a Comment