Dkt.
Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la
kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda
kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo
Akizungumza
kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika
amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa
inlocshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata
ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa
New York Marekani.
"Sasa
hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu alafu mimi nisepe, nikiwa
hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa
Mataifa Bara la Afrika, sasa ni world wide ofisi itakuwa New York,
nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR, hata mama Kevela
alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na
watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto
power, veto power ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa
projected na Urusi na mwenyewe Putin", amesema Dkt. Shika.
Dkt.
Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa
yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina
lake kupitishwa ikiwemo na Marekani
0 comments:
Post a Comment