Kamanda
mkoa wa kipolisi Tarime/Rorya, Henery Mwaibambe, amethibitisha kutokea
kwa tukio hilo na kusema mtuhumiwa amefunguliwa shtaka kituoni hapo
namba TAR/IR/5034/2017 na kuwa atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi
kukamilika.
Aidha,
Kamanda huyo aliongeza kuwa mtuhumiwa anatarajiwa kupelekwa mahakamani
kesho ili kujibu shtaka linalomkabili ikiwa ni pamoja na kumsababishia
maumivu makali mtoto huyo.
Akizungumzia
tukio hilo nyumbani kwake, mama mzazi wa mtoto huyo (jina
limehifadhiwa), amesema amelipokea kwa mshituko mkubwa tukio hilo ambapo
lilibainika Disemba 14, 2017 wakati mtoto aliposhindwa kula na kuanza
kuharisha mara kwa mara.
“Kugundua
kuwa mtoto wangu ameathirika na kitendo hicho ni baada ya kuwa
ameshindwa kula huku akiwa anaharisha mara kwa mara, kitendo ambacho
kilinishtua moyo wangu na mtoto hakuwa na dalili ya kuugua ikabidi
nianze kufanya ufuatiliaji wa kina ili kujua kilichompata,” alisema.
Ameongeza
kuwa tukio hilo amelipokea kwa masikitiko makubwa na kuwa hakuwa na
habari kuwa mwanaye wa miaka minne anaweza kutendewa kitendo cha kinyama
kiasi hicho na mtuhumiwa ambaye ni mpangaji mwenzake.
Akizidi
kufafanua, amesema kuwa baada ya kugundua mwanaye amekuwa akilawitiwa
mara nyingi kwa nyakati tofauti, alichukua hatua za kwenda kwa wataalamu
ili kuchukuliwa vipimo kwa ajili ya kijiridhisha.
“Hatua
nilizochukua baada ya kugundulika kuwa mwanangu alikuwa ameathirika kwa
muda mrefu ni kwenda kituoni polisi ili kutoa taarifa kwa hatua zaidi
kuchukuliwa dhidi ya mtuhumiwa,”alisema mama huyo..
”Baada
ya kwenda polisi ilibidi twende hospitalini kwa uchunguzi ambapo
daktari alisema hakuona dalili zozote ila nikasema kuwa haiwezekani kuna
mchezo unafanywa, andipo niliomba kwenda Bugando kwa uchunguzi zaidi
ambapo polisi walitoa askari wa kwenda kujiridhisha,” aliongeza.
Alibainisha wakati wakiwa Bugando, daktari aliyemfanyia vipimo alisema mtoto huyo amelawitiwa mara nyingi zaidi ya mwaka mmoja.
0 comments:
Post a Comment