Home » » Baba adaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachoma visu

Baba adaiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachoma visu

Unknown | Friday, December 29, 2017 | 0 comments
MWANAMUME mmoja amewaacha wanakijiji na mshangao mkubwa baada ya kudaiwa kuwaua wanawe wawili kwa kuwadunga kwa kisu kabla ya kujaribu kujiua katika mtaa wa Kiganjo Thika Kenya Jumanne usiku

Inasemekana kuwa James Kioho aliwadunga kisu mwanawe wa kiume mwenye umri wa miaka sita na wa kike mwenye umri wa miaka miwili nyumbani kwao mwendo wa saa mbili za usiku.

Kulingana na dadake, mwanamume huyo aliondoka mtaani humo mnamo Desemba 23 kwenda nyumbani kwa sherehe za Krismasi lakini akarejea pamoja na wanawe Jumanne alasiri.
Mwanamke huyo, ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema Bw Kioho alidaiwa kukorofishana na mkewe nyumbani kwao Naro Moru, kaunti ya Nyeri, kabla ya kuanza safari kurejea Thika.
Baadaye jioni dada huyo alisema Bw Kioho alimpigia mkewe simu akitisha kuwaua wanawe na kisha kujiua kwa kunywa sumu.
“Wifi yangu alinipigia simu ..... Hapo ndipo mimi na majirani wengine tuliamua kufika nyumbani kwa kakangu lakini kwa bahati mbaya tulipata amewaua watoto hao kisha akajaribu kujitoa uhai,” akasema.
Bw Julius Mulei ambaye pia ni jirani, alisema mwanamume huyo aliwasili mtaani humo pamoja na watoto hao Jumanne saa nane alasiri.
Aliwaambia wanahabari kwamba watoto hao walikuwa wenyewe furaha huku wakioenekana wakicheza nje ya nyumba yao.
“Lakini mwendo wa saa mbili za usiku watoto hao walianza kulia huku wakiomba usaidizi,” akasema Bw Mulei.
Alisema walipoenda kuangalia kile kilikuwa kikiendelea nyumbani kwao walimpata Bw Kioho akijaribu kujiua baada ya kuwaua watoto hao.
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG