Ilidaiwa
Bw Gideon Simiyu, alihudhuria tamasha ya mwanamuziki kutoka Uganda,
Jose Chameleon, katika kilabu cha Epic mkesha wa Krismasi akiwa na
mpenzi wake.
Alikasiirishwa
wakati mpenzi wake ambaye bado hajatambuliwa, alipoamua kusakata densi
na mwanamume mwingine kilabuni ndipo akajitia kitanzi Jumatano.
Kulingana
na Bw Isaac Wafula, ambaye ni binamu yake anayeishi kijiji cha Matisi,
marehemu alionekana mara ya mwisho katika soko la Matisi mnamo Jumapili
usiku akipigana na mpenzi wake walipokuwa wakirudi nyumbani.
“Alikuwa
mwenye hasira sana aliporudi nyumbani. Aliniambia waligombana na mpenzi
wake kwa sababu ya mwanamume ambaye mpenzi wake alikutana naye na
kucheza densi pamoja kilabuni. Baadaye alienda moja kwa moja hadi
chumbani mwake kisha akaondoka bila simu yake,” akasema Bw Wafula.
Aliongeza
kuwa katika siku ya Krismasi, marehemu aliandika ujumbe kwenye mtandao
wa kijamii wa Facebook kwamba wengi watamtamani ifikapo mwaka wa 2018.
Aliandika jumbe mbili kwenye mtandao huo kusema: “2018 nitaiona kweli? Mungu nisaidie.”
Mwingine ukasema: “Wallahi naona nikibaki 2017.”
Bw Dickinson Chelee, ambaye ni bawabu, alisema mwili wa marehemu ulionekana ukining’inia mtini ukiwa na kamba shingoni mwake.
Mkuu wa polisi wa Trans Nzoia, Bw Jackson Mwenga, alithibitisha kisa hicho na kusema upelelezi umeanzishwa.
“Tulitembelea
eneo la mkasa tukapata mwili wa marehemu Gideon Simiyu, ukining’inia
mtini. Tunashuku alijitoa uhai lakini tumeanzisha uchunguzi,” akasema.
Mwili
huo ulipelekwa kuhifadhiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kitale
ukisubiri kufanyiwa upasuaji kubainisha chanzo halisi cha kifo.
0 comments:
Post a Comment