Home » » Wafanyabiashara wapewa 'shavu' jijini Dodoma

Wafanyabiashara wapewa 'shavu' jijini Dodoma

Unknown | Wednesday, May 02, 2018 | 0 comments
Kampuni zinazotengeneza vifaa vya ujenzi zimeshauriwa kutumia fursa ya kufanya biashara hususani katika kipindi hiki ambacho serikali inahamia Dodoma.

Ushauri huo ulitolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi wakati alipokuwa akizungumzia juu ya maandalizi ya maonyesho kwa kampuni zinazotengeneza vifaa vya ujenzi na samani za ndani pamoja na wadau wa sekta ya ujenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa amezitaka kampuni hizo kutumia fursa ya ujio wa makao makuu kwa kujitambua, ili mashirika, taasisi na watu binafsi wanaojenga Dodoma wafahamu ni bidhaa gani bora kwa ajili ya ujenzi.

Maonyesho hayo yanafahamika kama Dodoma Builders Expo 2018, na alisisitiza kwamba fursa hiyo ni kubwa na wafanyabiashara wa vifaa vya ujenzi waitumie kuonyesha bidhaa bora.

Kunambi alisema ni kosa kulifananisha jiji la Dodoma na mikoa mingine nchini kwani linatakiwa kufananishwa na Jiji la Nairobi Kenya na Pretoria Afrika ya Kusini.

Kwa upande wake mratibu wa maonyesho hayo, Victor Simon alisema katika Jiji la Dodoma kuna vibarua na mafundi ambao wote wanachangamoto zinazofanana.

Mratibu huyo aliwataka makandarasi wa jiji hilo kuwatumia mafundi na vibarua wa Dodoma, na kuacha tabia ya kutumia wale wa kutoka maeneo mengine.

Alisema maonyesho hayo pia yanalenga kuwatambulisha na kuwaibua mafundi na vibarua na wanatarajia kuongeza ujuzi na kukuza vipato. 

Advertisement
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG