Home » » Serikali yapiga marufuku uuzaji wa mazao yakiwa bado shambani

Serikali yapiga marufuku uuzaji wa mazao yakiwa bado shambani

Unknown | Monday, May 07, 2018 | 0 comments
Serikali imewapiga marufuku wafanyabiashara, walanguzi na wakulima kuuza mazao yakiwa bado shambani na kusema pindi atakaebainika kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Hayo yamebainishwa leo Mei 07, 2018 Bungeni Jijini Dodoma kwenye kikao cha 23 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Naibu Waziri wa Kilimo Dkt. Mary Mwanjelwa na kusema kuwa ili kutatua tatizo hilo serikali inaanda mfumo maalumu ambao utatumika katika kuuza mazao kwa soko huria ili kuepusha hasara kwa wakulima.

"Uimarishwaji wa vyama vya msingi vya ushirika na vyama vikuu vya ushirika ili kupitia vyama hivyo wakulima waweze kuuza mazao yao na kujihakikisha soko la mavuno yao. Serikali itasimamia uzwaji wa mazao ya wakulima kwa njia ya minada ili kuweka kuweka ushindani wa bei na kumuwezesha mkulima kupata bei kubwa kama ilivyo katika zao la korosho", amesema Dkt. Mwanjelwa.

Advertisement
Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG