Nyota wa filamu nchini, Wema Sepetu amesema, hana bifu na Hamisa Mobetto, ila pia si rafiki yake.
Wasichana hao walikuwa marafiki lakini hivi karibuni zilienea taarifa kuwa wamegombana.
Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006 amesema hana tatizo na msichana huyo ila alimchukia baada ya kupata taarifa kuwa alikuwa akimuongelea vibaya kwa watu.
"Sina bifu na Hamisa ila siyo rafiki yangu kabisa kuna maneno aliniongelea mabaya… tena sio kwa kuhadithiwa, nilimsikia akiwa amerekodiwa… sasa nikaona huo ni unafiki kwa hiyo nikaona kila mtu achukue muda wake,"amesema Wema.
Amesema, akikutana na Hamisa hataki salamu na mwanamitindo huyo, kila mtu afanye mambo yake.
Hamisa amezaa na Naseeb Abdul ‘Diamond’ na hivi karibuni mwanamuziki huyo alitupia video ya wawili hao wakiwa kwenye mikao ya kimahaba.
Wema na Diamond walikuwa wapenzi, waliachana na kurudiana takribani mara mbili kabla ya kuachana tena kwa ugomvi mpaka kufikia hatua ya kutosalimiana.
Takriban miezi miwili iliyopita, Wema na Diamond walionekana pamoja na wenyewe wanadai wamekuwa marafiki wa kawaida si wapenzi tena.
0 comments:
Post a Comment