Home » » MBUNGE WA JIMBO LA MAKETE PROF NORMANI SIGARA KIN'G AMEKABIDHI ZAIDI YA MABATI 190 KUCHANGIA MAENDELEO YA MAKETE.

MBUNGE WA JIMBO LA MAKETE PROF NORMANI SIGARA KIN'G AMEKABIDHI ZAIDI YA MABATI 190 KUCHANGIA MAENDELEO YA MAKETE.

Unknown | Friday, April 27, 2018 | 0 comments

 Zaidi ya Mabati 190,yametolewa na MBUNGE WA JIMBO LA MAKETE PROF NORMAN ADAMSON SIGARA KING kuchangia shughuli za maendeleo katika Baadhi ya vijiji vya wilaya ya MAKETE.

Prof Normani sigara ,ametoa bati hizo akiwa katika ziara kwa baadhi ya vijiji vya jimbo la MAKETE lengo likiwa ni kuchangia shughuli za maendeleo,ambapo amechangia bati arobaini (40) kukamilisha ujenzi wa madarasa shule ya msingi MANGA,mabati 50 shule ya sekondary KITULO huku bati 50 zikikabidhiwa kwa shule ya msingi LUVULUNGE na kijiji cha MAGO bati 50.

Mh.Sigara pamoja na ziara ya kuona na ckuchangia shughuli za maendeleo,pia ametembelea kambi ya wachina wanaojenga barabara ya MAKETE -NJOMBE ambapo amewataka kutoa kipaumbele kwa wakazi wa MAKETE katika Kutoa ajira zote zinazo wezekana kwao kwa kuzingatia taaluma walizonazo na uwezo wao badala ya kuwatumia zaidi watu kutoka nje ya wilaya ya MAKETE.




Kwa upande wao baadhi ya Wananchi katika maeneo yaliyo tembelewa na Mh. Mbunge wamemshukuru Mbunge Pamoja na kuahidi kumpa ushirikiano katika kujenga wilaya ya MAKETE.

Share this article :

0 comments:

Post a Comment

 
Support : Copyright © 2018. AFRICAN NEWS BLOG - All Rights Reserved
Imetengenezwa na Edwin Moshi
Inaendeshwa na AFRICAN NEWS BLOG