Kufuatia aliyekuwa diwani wa kata ya isapulano
bwana ALFONCE MBILINYI kujiuzulu kutoka chama cha demokrasia na maendeleo
[CHEDEMA] kuhamia chama cha mapinduzi [CCM]Wananchi wa kata ya isapulano
wilayani makete mkoani njombe wameaswa
kutunza vitambulisho vya kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio
wa diwani wa kata hiyo.
Afisa uchaguzi wa wilaya ya makete bwana
GREGORY EMANUEL amesema kuwa vitambulisho hivyo vitasaidia kupiga kura ili
kuweza kumchagua diwani mwingine kutokana na diwani wa awali kujiuzulu na kuhamia
chama kingine na kuacha nafasi hiyo wazi.
Wakati huo huo Gregory amesema kuwa katika wilaya ya makete kuna
nafasi 12 za wenyeviti wa vitongoji ziko wazi na nafasi 11 za wenyeviti wa vijiji ziko wazi kama halmashauri inajipanga
kufanya uchaguzi sehemu hizo na kuwapata viongozi kwa mujibu wa sheria.
Gregory amesema uchaguzi wa marudio utafanyika mpaka pale tume ya taifa ya
uchaguzi itakapo toa taarifa za kufanyika uchaguzi huo wa udiwani.
0 comments:
Post a Comment