JAMII IMESHAURI KUJITOKEZA KWA AJILI YA KUCHANGIA DAMU ILI KUOKOA MAISHA YA BINDDAMU WANAOHITAJI MSAADA WA DAMU .
MKUU WA KITENGO CHA DAMU PEMBA DR ABDI KASSIM HAMAD AMESEMA SUALA LA KUCHANGIA DAMU NI HIARI , LAKINI MAHITAJI YA DAMU NI KILA MMOJA ANAYEFIKWA NA TATIZO .
AKIZUNGUMZA WAKATI NA WAUMINI WA KANISA LA SABATO KISIWANI PEMBA HUKO NGERENGERE JESHINI , WAKATI WA ZOEZI LA UCHANGIAJI WA DAMU AMEWATAKA WANANCHI KUWATUMIA WATAALAMU KWA AJILI YA KUPIMA AFYA NA KUACHA KUKIMBILIA KWA WAGANGA WA KIENYEJI .
NAYE MCHUNGAJI WA KANISA HILO PEMBA PASKALI MTWANA , AMESEMA UWAMUZI WA KUTOA KUCHANGIA DAMU KWA WAUMINI WA KANISA HILO NI KUTEKELEZA KWA VITENDO MAANDIKO .
AMESEMA KANISA LITAENDELEA KUUNGA MKONO JUHUDI ZA SERIKALI KATIKA KUTATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI HUSUSANI MAHITAJI YA DAMU .
0 comments:
Post a Comment